Jumanne 6 Mei 2025 - 12:45
Mwalimu wa Hawza: Hawza ya Qum Ipo Mstari wa Mbele katika Kuipanua Tawhidi na Kupambana na Tw'aghuti (Shet'ani)

Hujjatul Islam Abidiyan amesema: Kinyume na baadhi ya hawza ambazo zimefuata njia potofu ya kisekula na hazikuwa na uelewa sahihi wala basira (maono) ya kina kuhusu misheni asilia, Hawza ya Qum imekuwa mstari wa mbele katika kupanua Tawhidi na kupambana na tw'aghuti.

Shirika la Habari la Hawza - Hujjatul Islam Sayyid Reza Abidiyan, katika mahojiano na mwandishi wa habari wa shirika la habari la Hawza, alizungumza kuhusu mafanikio ya karne moja ya Hawza ya Qum na alisema: “Mojawapo ya misheni muhimu sana ya Mitume wote wa Mwenyezi Mungu na Maimamu watoharifu (a.s) ilikuwa ni kupanua Tawhidi na kupambana na shirki, dhulma na tw'aghuti,” jambo ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu amelieleza katika aya nyingi, na mwenendo wa vitendo na wa kauli wa wajumbe wote wa Mwenyezi Mungu unaonyesha wazi misheni hiyo muhimu.

Mwalimu huyo wa hawza alieleza kuwa: Kwa kuingia katika zama za ghaiba, misheni hii ya kimungu mekuwa mikononi mwa maulamaa wa dini, na katika vipindi mbalimbali vya historia tumeona juhudi za jihadi kwa maulamaa wengi waliotumikia njia ya kusambaza Tawhidi, kupambana na tw'aghuti, na kueneza ustaarabu wa Kiislamu.

Aliendelea kusema: Kwa kufufuliwa Hawza ya Qum kupitia juhudi za marehemu Ayatullahil Uzma Haj Abdulkarim Ha’iri Yazdi, tumeshuhudia kulelewa na kutumwa kwa maulamaa wengi wa dini katika maeneo yote ya nchi na hata duniani kote, wamekuwa ni wahubiri na watoa ujumbe wa fikra ya Tawhidi, na wamekuwa wakiwaalika watu kusimama imara na kujitolea katika kupambana na tw'aghuti. Hii ilifikia kilele baada ya kuwasili kwa Imam Khomeini (r.a) mjini Qum na Mapinduzi ya Kiislamu, ambapo palitokea mwamko mkubwa mno katika uwanja huu.

Hujjatul Islam Sayyid Reza Abidiyan alieleza: Leo hii, baada ya kupita zaidi ya miaka mia moja tangia kufufuliwa kwa Hawza tukufu ya Qum, wahubiri wa Tawhidi, waenezaji wa ustaarabu mpya wa Kiislamu, na wapandikizaji wa fikra ya Kiislamu, ambao wote kwa pamoja wamebahatika kuwa wanafunzi wa Hawza hii tukufu, si tu ndani ya Iran bali pia katika nchi nyengine duniani kote, wanatekeleza jukumu lao la kimungu.

Hujjatul Islam Abidiyan, kwa kubainisha kuwa Hawza ya Qum, kupitia kuanzishwa kwa taasisi mbalimbali maalum na pia kuanzisha zaidi ya fani mia nne maalumu pamoja na makumi ya mihadhara ya masomo ya "darsa al-kharij" ya fiqhi ya kisasa, na kulea wanafunzi wa dini wanaojua lugha, imekuwa na mchango mkubwa sana katika kutoa huduma za kielimu, kuunda taasisi za kielimu na kuwa na nafasi ya kimataifa katika nyanja za kimungu, alikumbushia kuwa: Shughuli mbalimbali ambazo Hawza ya Qum inatekeleza katika nyanja mbalimbali, hasa katika uwanja wa kimataifa, ni jambo lisilofichika kwa mtu yeyote.

Mwalimu huyo wa hawza, kwa kubainisha kuwa kinyume na baadhi ya hawza ambazo zimefuata njia potofu ya kisekula na kukosa uelewa sahihi na basira ya kina kuhusu misheni mbili tajwa hapo juu, Hawza ya Qum iko mstari wa mbele katika kupanua Tawhidi na kupambana na tw'aghuti, alisema: Bila shaka, tw'aghuti wa leo huenda akatofautiana na tw'aghuti wa jana, lakini kwa mujibu wa misheni ya kimungu iliyotajwa katika Qur’an na Sunnah, pamoja na tamko la "Hatua ya Pili ya Mapinduzi ya Kiislamu", na mfumo wa fikra wa maulamaa kama Imam Khomeini (r.a), Muhhaqqiq Karaki, Allamah Misbah, na wengine, hawza hii inaendelea kutoa huduma duniani kote. Pamoja na kusambaza itikadi ya Tawhidi, inaendelezea pia roho ya kujitolea, kusimama kidete, na jihadi ya kupambana na tw'aghuti, na inaendelea kuijenga fikra ya Tawhidi na jihadi ndani ya nyoyo za watu.

Mwisho wa ujumbe.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha